You are currently viewing MASOKO YA TUMBAKU CHUNYA NI KIDIGITALI; HAIJAPATA KUTOKEA TANZANIA

MASOKO YA TUMBAKU CHUNYA NI KIDIGITALI; HAIJAPATA KUTOKEA TANZANIA

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amesema kutumia mizani za kidigitali katika masoko ya zao la Tumbaku mwaka 2026 kutasaidia kuweka vizuri Kumbukumbu kwa pande zote zinazohusika kwenye soko yaani mkulima na mnunuzi, jambo litakaloleta usawa, uwazi na ufanisi wa soko

Ametoa kauli hiyo 27.04.2026 wakati akizungumza na wadau wa zao la Tumbaku waliokuwa wameketi katika ukumbi wa ghala la Chama cha Msingi Lupatingatinga wakijadiliana maandalizi ya soko la Tumbaku kwa mwaka 2026

“Suala la vipimo halijawahi kumwacha mtu salama, hivyo niwahakikishieni wajumbe wote wa kikao hiki kwamba kupitia mizani hizi zitasaidia sana kuweka sawa kumbukumbu za kilichoenda sokoni na kilichouzwa, Na ninaamini mizani hizi zitakuwa zinakaguliwa kwa mujibu wa utaratibu ili kuhakikisha haki stahiki inapatikana” Alisema Mhe Batenga

Aidha, Batenga aliwapongeza sana viongozi wa Chama cha kikuu cha Ushirika 9CHUTCU)  kupitia mwenyekiti wa bodi kwa kusimamia wakulima waliopo katika vyama vya ushirika, jambo ambalo limepelekea hata kufikia mabadiliko kutoka kutumia mizani za analogia na sasa soko la mwaka 2026 mizani za digitali zitatumika

Mrajisi msaidizi wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Richard Elia amesema wilaya ya Chunya itakuwa wilaya ya kwanza kutumia mizani ya kidigitali nchini katika masoko ya Tumbaku kwakuwa mikoa yote inayolima zao la Tumbaku nchini bado hutumia mizani za analogia hivyo amewataka wanachunya kuendelea kutembelea kifua mbele kwakufikiwa na mabadiriko hayo

“Lakini kwenye zao la Tumbaku kwa maana ya mikoa yote ionayolima Tumbaku Tanzania, nafikiri Chunya ndo inatakuwa wilaya ya Kwanza kutumia mizani ya kidigitali hivyo Chunya jipongezeni sana kwa hatua hii ya mabadiliko” Alisema Richard

Bwana Richard ameongeza kuwa kupitia mizani hizi, zitarahisisha sana zoezi la utunzaji wa Kumbukumbu lakini pia upatikanaji wa Kumbukumbu kwa wadau wote wanaohusiana na zao la Tumbaku, jambo ambalo litaendelea kurahisisha utendaji kazi katika mchakato wote wa kilimo cha Tumbaku nchini na hatimaye kuwahudumia wakulima kwa urahisi na kwa wakati

Zaidi ya mizani thelasini na nane zimenunuliwa kwa lengo la kutumika katika Masoko ya Tumbaku mwaka 2026 yanayotaraji kuanza hivi karibu lengo kubwa ikiwa ni kuhakikisha haki, uwazi na usawa vinazingatiwa kwa pande zote mbili yaani muuzaji (Mkulima) na mnunuzi (Kampuni) ili kuleta tija kwa wananchi wa Chunya na Taifa kwa Ujumla

Leave a Reply